Home Sports BREAKING:RASMI SIMBA YAMFUTA KAZI PABLO FRANCO

BREAKING:RASMI SIMBA YAMFUTA KAZI PABLO FRANCO

LEO Mei 31 Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu Pablo Franco Martin raia wa Hispania.

Katika taarifa iliyotolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez, imeeleza kuwa katika kipindi chote cha kumalizia msimu, timu itakuwa chini ya kocha msaidizi, Seleman Matola.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa pia timu hiyo imevunja mkataba na kocha wa viungo, Daniel De Castro Reyes.

Pablo alikuja Bongo kuchukua mikoba ya Didier Gomes ambaye aliweza kubwaga manyanga kwenye timu hiyo baada ya kushindwa kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa

Previous articleWAYDAD WATWAA TAJI LA TATU LIGI YA MABINGWA AFRIKA
Next articleSIMBA YAFANYA KIKAO NA KOCHA MPYA SAA 72