Home Sports YANGA WAACHANA RASMI NA KIUNGO NTIBANZOKIZA

YANGA WAACHANA RASMI NA KIUNGO NTIBANZOKIZA

 LEO Mei 30,2022 Klabu ya Yanga imetangaza rasmi kuachana na mchezaji wake Saido Ntibazonkiza baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa miaka miwili.

Katika taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga,imeeleza kuwa Ntibazonkiza amemaliza utumishi wake ndani ya klabu hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza namna hii:”Uongozi wa Klabu ya Yanga unapenda kutoa shukrani za dhati kwa mchezaji wetu Said Ntibanzokiza kwa utumishi wake ndani ya klabu ya Klabu ya Yanga.

“Said Ntibanzokiza amemaliza mkataba wake leo Mei 30 alioutumikia kwa miaka miwili.

“Yanga tunamshukuru kwa kipindi ambachi alikuwa pamoja nasi na tunatakia kila la kheri na mafanikio katika maisha yake ya soka nje ya Klabu ya Yanga,”

Previous articleMASTAA WATATU SIMBA WAWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA
Next articleMRITHI WA PABLO ATUA DAR,NDANI YA SPOTI XTRA JUMANNE