
HELLO, MWENDELEZO WA MAYELE SOMO KWA WAZAWA
MWENDELEZO mzuri wa kucheka na nyavu upo kwenye miguu ya Fiston Mayele kinara wa utupiaji mabao ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa ametupia mabao 11. Alipowatungua Polisi Tanzania hakushangilia kwa mtindo wake wa kutetema bali alionekana kwa kitendo chake akipiga simu kisha akaongea na kuanza kushangilia. Wanasema alikuwa anawapigiwa watani zake wa jadi pale Mwanza…