Home Sports YANGA:POLISI TANZANIA WANAKUJA MACHINJIONI

YANGA:POLISI TANZANIA WANAKUJA MACHINJIONI

ALLY Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wapinzani wao Polisi Tanzania wanawafuata machinjioni Uwanja wa Mkapa jijini Dar hivyo wajiandae ‘kufa’.

Yanga kwenye msimamo ipo nafasi ya kwanza ikiwa imekusanya pointi 38 baada ya kucheza mechi 15 mchezo wake uliopita Uwanja wa Mkapa ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho na iliibuka na ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Kurugenzi.

Polisi Tanzania inanolewa na Mwinyi Zahera ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha Yanga ambacho kwa sasa kipo chini ya Kocha Mkuu Nasreddine Nabi.

Kamwe amesema: “Jumamosi tunacheza na Polisi Tanzania, wanakuja machinjioni hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia burudani na tunaamini kila kitu kitakuwa sawa.”

Mchezo wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ubao ulisoma Polisi Tanzania 1-2 Yanga.

Miongoni mwa wachezaji ambao wamefanya mazoezi ya mwisho ni pamoja na Eric Johora, Kibwana Shomari, Dickson Job.

Previous articleUMAFIA MZITO, PHIRI, BOCCO WAACHIWA MSALA GEITA GOLD
Next articleYANGA YAITULIZA POLISI TANZANIA, MAYELE NAMBA MOJA