Home Sports YANGA YAITULIZA POLISI TANZANIA, MAYELE NAMBA MOJA

YANGA YAITULIZA POLISI TANZANIA, MAYELE NAMBA MOJA

NYOTA Fiston Mayele nyota namba moja wa kikosi cha Yanga leo amepachika bao lake la 11 ndani ya Ligi Kuu Tanzania.

Katupia bao hilo wakati wakishinda mabao 3-0 dhidi ya Polisi Tanzania kwenye mchezo uliochezwa Uwanjawa Mkapa.

Dakika 45, vijana Polisi Tanzania chini ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera walikomaa na kulinda ngome isifungwe huku wao wakikwama kuitungua Yanga.

Kipindi cha pili mabao yote matatu yalifungwa ambapo Jesus Moloko alifungua pazia dakika ya 46 kisha Mayele dakika ya 77 na Mzize alipachika bao la tatu dakika ya 85.

Mchezo wa leo nyota wa Polisi Tanzania alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano ambaye ni Amborose Awio.

Previous articleYANGA:POLISI TANZANIA WANAKUJA MACHINJIONI
Next articleKITAWAKA FAINALI KOMBE LA DUNIA LEO, PATA ODDS ZA MERIDIANBET