Mchezo wa mtoano wa ligi kuu NBC mkondo wa kwanza wa Mbeya City dhidi ya Tanzania Prison umemalizika ubao wa Uwanja wa Sokoine umesoma Mbeya City 2-0 Tanzania Prisons.
Wababe hawa wawili kutoka Mbeya wanapambania nafasi ya kubaki ndani ya ligi baada ya kumaliza ligi wakiwa katika nafasi zinazostahili wao kucheza mchezo wa mtoano.
Mbeya City ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya 14 na pointi 30 huku Tanzania Prisons nafasi ya 13 na pointi 32 baada ya mechi 30.
Kwenye mchezo wa leo ni Said Naushad alifungua pazia la kufunga dakika ya 15 na Hija Shamte dakika ya 87 zikiwa zimesalia dakika 3 mpira kufika ukingoni alipachika bao la pili.
Mshindi wa jumla atapatikana kwenye mkono wa pili mchezo unaotarajiwa kuchezwa Julai 8,2026.
Timu mbili ambazo zimeshuka daraja moja kwa moja zitashiriki Championship ni Mtibwa Sugar na KMC FC.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, itakuwa mezani Julai 10,2026 jiandae kuipata.