Home Uncategorized GEITA GOLD AKILI ZOTE KWA SIMBA

GEITA GOLD AKILI ZOTE KWA SIMBA

 KOCHA Mkuu, Felix Minziro ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2021/22 wakati Minziro akikinoa kikosi hicho mchezo wao wa ligi walipokutana ubao ulisoma Geita Gold 1-1 Simba.

Kwa Geita Gold bao lilipachikwa kimiani na George Mpole ambaye alikuwa mfungaji bora alipogotea kwenye mabao 17 kibindoni.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Geita Gold, Hemed Kivuyo ameweka wazi kuwa benchi la ufundi limekamilisha maandalizi kwa asilimia kubwa na wanachohitaji ni ushindi.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu Simba na tunatambua kwamba ni timu kubwa lakini benchi la ufundi limefanya kazi kubwa kuandaa kikosi na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo.

“Akili ni kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona namna gani tunatoa burudani kwenye mchezo wetu,”.

Kuziona shoo za Geita Gold v Simba Uwanja wa CCM Kirumba kwa upande wa mzunguko ni 5,000, VIP B ni 10,000 na VIP A ni 20,000.

Previous articleKIUNGO SIMBA RAIA WA MALI KUIBUKIA MBELE YA GEITA GOLD
Next articleMOROCCO HUZUNI TUPU, CROATIA FURAHA