Home Uncategorized KIUNGO SIMBA RAIA WA MALI KUIBUKIA MBELE YA GEITA GOLD

KIUNGO SIMBA RAIA WA MALI KUIBUKIA MBELE YA GEITA GOLD

KIUNGO wa kazi ngumu ndani ya kikosi cha Simba,Sadio Kanoute raia wa Mali anatarajiwa kurejea kuikabili Geita Gold kwenye mchezo wa ligi.

Nyota huyo alikosekana kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Eagle FC uliochezwa Uwanja wa Mkapa kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopata baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano mchezo dhidi ya Coastal Union.

Adhabu yake imegota mwisho na alishuhudia timu hiyo ikishinda mabao 8-0 na kutinga raundi ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho.

 Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema kuwa walimkosa mchezaji huyo kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hivyo watakuwa naye kwenye mchezo wa ligi Desemba 18 dhidi ya Geita Gold.

“Alikosekana kwenye mchezo dhidi ya Eagle kwa kuwa alikuwa na kadi mbili za njano, hivyo adhabu yake imeisha tunaamini kwamba tutakuwa naye kwenye mchezo ujao wa ligi,”.

Kiungo huyo kacheza mechi 10 za ligi akiwa ameyeyusha dakika 680 ni chaguo la kwanza la Mgunda.

Leo Simba inatarajiwa kushuka Uwanja wa CCM Kirumba kusaka pointi tatu muhimu kwenye mchezo wao wa ligi.

Kanoute ni miongoni mwa wachezaji ambao jana Desema 17 walifanya mazoezi ya mwisho kuikabili Geita Gold.

Previous articleKITAWAKA FAINALI KOMBE LA DUNIA LEO, PATA ODDS ZA MERIDIANBET
Next articleGEITA GOLD AKILI ZOTE KWA SIMBA