Home International MOROCCO HUZUNI TUPU, CROATIA FURAHA

MOROCCO HUZUNI TUPU, CROATIA FURAHA

MASHABIKI wa Croatia walikuwa na furaha huku wale wa Morocco wakiwa na huzuni baada ya kupoteza mchezo wao kweye Kombe la Dunia.

44,137 ni idadi ya mashabiki ambao walikuwa ndani ya Uwanja wa Taifa wa Khalifa kushuhudia mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu wa Kombe la Dunia 2022 Qatar ambaye ni Croatia.

Matumaini ya Morocco kuibukia kwenye nafasi ya tatu yalibuma baada ya kupoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 2-1.

Bao la ufunguzi kwa Croatia yenye Luka Modric lilipachikwa na Josko Gvardiol dakika ya 7 ambapo liliwekwa usawa na nyota wa Morocco Achraf Dari dakika ya 9.

Bao la pili lilipachikwa na nyota wa Croatia dakika ya 42 ambaye ni Mislav Orsic aliyezima ndoto za Morocco jumlajumla.

Ni faulo 24 zilishuhudiwa zikifanyika kwenye mchezo huo ambapo Croatia wao walikuwa nazo 13 na Morocco kutoka Afrika wao walikuwa nazo 11 na kadi mbili za njano pekee zote zikiwa mali ya Morocco.

Leo ni leo ambapo fainali inatarajiwa kuchezwa kati ya Ufaransa na Argentina.

Previous articleGEITA GOLD AKILI ZOTE KWA SIMBA
Next articleFAINALI YA KIBABE LEO KOMBE LA DUNIA