Home Sports NABI: TULIENI, HAO WAARABU NAWAJUA NJE NDANI

NABI: TULIENI, HAO WAARABU NAWAJUA NJE NDANI

KOCHA Mkuu wa Yanga Mtunisia, Nasreddine Nabi amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo, kupangwa na US Monastir FC ya nchini Tunisia katika kundi moja hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga imepangwa pamoja katika Kundi D, zikiwa na timu za Union Sportive Monastery ya nchini Tunisia, TP Mazembe ya DR Congo na Real Bamako ya huko Mali ambazo zitacheza nyumbani na ugenini.

Hiyo itakuwa mara ya pili kwa Yanga kwenda kucheza nchini Tunisia kwani katika mechi ya mtoano ya shirikisho walipangwa kukipiga na Club Africain ya nchini humo na walishinda bao 1-0 na kuwaondosha Waarabu hao.

Akizungumza na Championi Jumatano, Nabi alisema kuwa, timu za kutoka Uarabuni zinaogopwa lakini kwake hana hofu kwani anazifahamu vizuri Nabi alisema kuwa timu hiyo, ya US Monastery anaifahamu vizuri kwani inatokea mtaani kwake ambako yeye anaishi na familia hivyo hana hofu kabisa.

Alisema kuwa anazijua mbinu zote ambazo wanazitumia kwani mara kadhaa aliwahi kupita kwa ajili ya kuifundisha na kuitazama yeye akiwa huko nyumbani kwao Tunisia.

Aliongeza kuwa nguvu anazielekeza kwa timu nyingine hizo ambazo zipo kundi moja ikiwemo TP Mazembe ya DR Congo.

“US Monastir inapotokea  ndio nimetokea mimi ambayo ipo mtaani kwangu ninapoishi huko Tunisia, hivyo ninaijua vizuri sana, hivyo sitateseka kuzijua mbinu zao na wachezaji wao hatari.

“Niliwahi kuifundisha na kuitazama katika michezo yao ya ligi na mashindano mingine, hivyo mashabiki wasiogopeshwe na timu hiyo ambayo inatajwa ndio tishio katika kundi letu,” alisema Nabi.

Previous articleFURAHA YA KUPOKEA BAJAJI YA MERIDIANBET IMEMFANYA ALIE
Next articleBOSI SIMBA: MANZOKI NDIYO, BOBOSI HAPANA