Home Sports MZUNGUKO WA PILI YANGA KUJA KIVINGINE

MZUNGUKO WA PILI YANGA KUJA KIVINGINE

CEDRIC Kaze, kocha msaidizi wa Yanga amesema kuwa mzunguko wa pili watakuwa tofauti kwenye upande wa kasi ya ufungaji wa mabao pamoja na ulinzi.

Timu hiyo imekamilisha mzunguko wa kwanza ikiwa imepoteza mchezo mmoja kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu na inaongoza ligi ikiwa na pointi 38.

Kaze amesema kuwa kukamilisha mzunguko wakiwa wanaongoza ni jambo kubwa hivyo watakuja na mbinu tofauti mzunguko wa pili.

“Unaona tumekamilisha mzunguko wa kwanza tukiwa ni namba moja na sasa tunakwenda kuanza mzunguko wa pili tunaamini wapinzani wetu watakuwa na kasi zaidi kwa kuwa wamepata mud wa kutufuatilia ni lazima tujipange.

“Ukweli ni kwamba ligi ina ushindani mkubwa hilo linatufanya nasi tuwe makini kwenye mechi zijazo na kufanya mambo kwa utofauti na upekee kwenye kusaka ushindi, mashabiki wawe pamoja nasi,” amesema Kaze.

Kesho timu hiyo ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Polisi Tanzania unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Previous articleSIMBA NDANI YA MWANZA KUIVUTIA KASI GEITA GOLD
Next articleVIDEO: KIMATAIFA WANANCHI WAAMBIWA HAWATOBOI