
NYOTA BARCELONA ASAINI ASTON VILLA
KIUNGO mshambuliaji wa FC Barcelona, Phillipe Coutinho amejiunga kwa mkopo kwenye klabu ya Aston Villa hii baada ya Villa kudhibitisha kupitia mitandao yake ya kijamii juu makubaliano ya timu zote mbili juu ya sahihi ya Mbrazili huyo. Coutinho anarejea tena nchini Uingereza baada ya kuondoka kwenye majira ya joto mwaka 2018 alipojiunga na miamba ya Uhispania,…