KIUNGO mshambuliaji wa FC Barcelona, Phillipe Coutinho amejiunga kwa mkopo kwenye klabu ya Aston Villa hii baada ya Villa kudhibitisha kupitia mitandao yake ya kijamii juu makubaliano ya timu zote mbili juu ya sahihi ya Mbrazili huyo.
Coutinho anarejea tena nchini Uingereza baada ya kuondoka kwenye majira ya joto mwaka 2018 alipojiunga na miamba ya Uhispania, FC Barcelona, akitokea Liverpool.
Villa na Barcelona watashirikiana kulipa mshahara wa Mbrazili huyo anayepokea Euro 380,000 sawasawa na shilingi milioni 992,357,604 za Kitanzania akiwa na Barca na sasa vilabu hivyo vitamlipa Euro 190,000 sawa na pesa taslimu za kitanzania 496, 178,802.
Akiwa na umri wa miaka 29, Coutinho amewahi kucheza pamoja na kocha wa Villa, Steven Gerrard wakiwa Liverpool kwa muda wa miaka miwili na nusu, jambo ambalo linasadikika kuwa limemvutia kiungo huyo kujiunga na timu hiyo aliyowahi kuhudumu Mtanzania, Mbwana Samatta.