WAKIWA Uwanja wa Stamford Bridge, Liverpool ilikwama kusepa na pointi tatu mbele ya Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu England.
Watajilaumu wenyewe kwa kuwa walipata mabao ya mapema ndani ya dakika 30 za mwanzo kupitia kwa Sadio Mane dakika ya 9 na Mohamed Salah dakika ya 26.
Hao Chelsea wanaonolewa na Thomas Tuchel walipindua meza kupitia kwa Mateo Kovacic dakika ya 42 na Christian Pulisic dakika ya 45+1.
Liverpool inafikisha pointi 42 ikiwa nafasi ya tatu huku Chelsea ikiwa nafasi ya pili na pointi 43 baada ya kucheza mechi 21 huku Liverpool ikiwa imecheza mechi 20.
Vinara ni Manchester City wenye pointi 53 baada ya kucheza mechi 21.