Home Sports NYONI KUACHWA SIMBA,JEMBE JIPYA HILI KUTUA SIMBA

NYONI KUACHWA SIMBA,JEMBE JIPYA HILI KUTUA SIMBA

IMEELEZWA kuwa mabosi wa Simba wamefikia maamuzi ya kuachana na kiungo mshambuliaji wao Mmalawi, Duncan Nyoni na kumalizana na kiungo Mzambia, Samuel Sikaonga.

Nyoni aliungana na Simba mwanzoni mwa msimu huu, kwa mkataba wa miaka mitatu, akitokea Silver Strikers ya Malawi, lakini ameshindwa kuonyesha kiwango bora ndani ya timu hiyo jambo linalodaiwa kuwapelekea mabosi wake kumfungashia virago.

Chanzo kutoka Simba kimeeleza kwamba, baada ya uongozi wa Simba kujadiliana kwa kina matakwa ya ripoti ya Kocha Mkuu Pablo Franco, umelazimika kukatisha mkataba na Nyoni ili utoe nafasi kwa kiungo Samuel Sikaonga.

“Ripoti ya kocha Pablo imeleta mabadiliko na maamuzi mazito sana ndani ya Bodi ya Wakurugenzi, hasa upande wa kamati ya usajili, ambapo umekata majina takriban matatu ya nyota wetu na kuachana nao rasmi akiwemo Nyoni.

“Kocha hajaridhishwa na uwezo wa Nyoni, jambo ambalo ameipa kamati ya usajili kutafuta mbadala wake, ambapo wao wameamua kumng’oa rasmi na kuingiza jina la Sikaonga ambaye atahudumu moja kwa moja katika nafasi ya Taddeo Lwanga,” kilisema chanzo hicho.

Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu hivi karibuni alisema kuwa kuhusu usajili wataweka wazi taarifa mambo yatakapokamilika.

Previous articleJANUARI 3,MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU
Next articleLIVERPOOL WAKWAMA KUSEPA NA POINTI TATU DARAJANI