>

WAPINZANI WA SIMBA KIMATAIFA WANATAKA KUTINGA ROBO FAINALI

KLABU ya US Gendarmerie ya Djibouti imesema imepangwa kundi zuri na Simba SC ya Tanzania hivyo wanao uhakika mkubwa wa kusonga mbele katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Droo ya makundi imepangwa nchini Misri ikiwa ni tayari kwa ajili ya kuweza kushuhudia mpambano wa kusaka taji hilo mwaka mpya wa 2022 na Tanzania inawakilishwa na Simba.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Zakariou Ibrahim amesema kuwa wapo kwenye kundi zuri na wanaamini kwamba watafanya vizuri na kusonga mbele.

“Tupo katika kundi lililopangwa vizuri lenye timu tatu kubwa ambazo ni RS Berkane iliyowahi kutwaa taji hili, Simba ambao wamekuwa wakicheza vyema katika Ligi ya Mabingwa pamoja na Asec Mimosas ambao wamekuwa wakishiriki mashindano haya.

“Malengo yetu ni rahisi tu, kumaliza tukiongoza na kufuzu hatua ya robo fainali. Tunaweza kufanya hivyo. Tunatakiwa kurudi katika mstari na kujituma pasipo kudharau taarifa yoyote muhimu,” amesema Zakariou.

20/2/2022 Simba inatarajiwa kumenyana na timu hiyo ambapo itaanzia ugenini kabla ya kurudi Uwanja wa Mkapa 03/04/2022.