MSHAMBULIAJI wa AC Milan, Zlatan Ibrahimovic hajaonesha kukubali uwezo wa mfalme wa Soka kutoka nchini Brazil Pele ambaye anatajwa kuwa ni nyota bora wa muda wote.
Licha ya Pele kuzungumzwa kufungwa magoli zaidi ya 1000 katika kipindi cha uchezaji wake, Zlatan haonekani kutishwa na rekodi hizo.
“Kama ningecheza enzi za Pele, ningefunga mabao 3000. Hakukuwa na sheria kali. Hakukuwa na kuotea (offside). Hakukuwa na VAR.
“Naamini bila offside ningefunga katika kila mechi, kitu pekee kingemzuia Zlatan asifunge ingekuwa majeruhi, bado sihesabu magoli yake Pele kwa sababu mengi yalikuwa ni magoli ya kuotea hata sijisumbui kumsikiliza anaposema yeye ni bora kuliko Ronaldo, Messi na Mimi,” amesema Zlatan.