KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco ameweka wazi kuwa sababu kubwa ya timu hiyo kuachana na baadhi ya
mastaa akiwemo kiungo, Ibrahim Ajibu aliyejiunga na Azam ni kuwaambia wazi kuwa hawakuwa na nafasi ndani ya kikosi chake.
Simba ilitangaza rasmi Desemba 30,2021 siku ya Alhamisi kusitisha mkataba na Ajibu kwa kile kilichoelezwa kuwa ni makubaliano ya pande zote mbili, ambapo nyota huyo tayari ametangazwa kusaini mwaka mmoja ndani ya kikosi cha Azam.
Akizungumza naSaleh Jembe, kocha Pablo amesema: “Ni kweli tulifikia muafaka wa kuachana na baadhi ya wachezaji wa kikosi chetu na hii ni kutokana na ukweli kuwa nilikaa na wachezaji hao na kuwaweka wazi kuwa wasingekuwa na nafasi kwenye kikosi changu.
“Lakini pia baadhi yao walishindwa kufikia matarajio yao binafsi na ya klabu, hivyo kama wanadamu ni lazima pia tuangalie faida ya pande zote mbili na ndiyo sababu ya kuachana nao.
“Ajibu ni mchezaji mzuri nina amini huko ambapo yupo benchi la ufundi litajua namna ya kuweza kufanya naye kazi kwa kuwa hayupo kwenye kikosi chetu,”.