Baada ya kushuhudia matamasha ya Simba Day na Yanga Day sasa ni zamu ya kuhamia uwanjani kwenda kumtafuta Bingwa ambaye ataondoka na Ngao ya Jamii. Je nani ataondoka na Kombe hilo?. Ingia Meridianbet na ubashiri sasa.
Mechi ya Simba dhidi ya Yanga kwenye Ngao ya jamii ni mchezo wa ufunguzi rasmi wa msimu mpya wa ligi kuu yaani 2026/2027 ambapo mechi hii itapigwa kule visiwani Zanzibar huku kila timu ikihitaji kuondoka na ushindi kwenye mechi hii.
Yanga anaingia kama bingwa mtetezi wa Kombe hili ambalo alilitwaa msimu uliopita baada ya kushinda kwa bao 1-0, wakati kwa upande wa Simba wao wanaingia uwanjani wakihitaji kulipa kisasi. Lakini je Wekundu hao wa Msimbazi wanaweza kufurukuta kwenye timu hiyo ambao inaonekana kuwa imara kwa miaka kadhaa?
Young Africans ambao ni mabingwa mara tano mfululizo kwenye ligi wanapewa nafasi kubwa ya kufanya vyema kwenye mechi hii kutokana na uimara ambao wameendelea kuuonesha ndani ya misimu hii. Timu hii sasa imeanza msimu mpya wakiwa na kocha mpya ambaye ni Manqoba Mngqithi ambaye sasa atakinoa kikosi hicho cha Wananchi.
Lakini pia Meridianbet inakwambia tengeneza mkwanja kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Manqoba ambaye ni kocha waliyemtoa Afrika Kusini ambaye amevinoa vilabu mbalimbali akihudumu katika nafasi mbalimbali ikiwemo Mamelodi Sundwons, alikuwa kocha mkuu wa timu ya Lamontville Golden Arrows kabla hajajiunga na Yanga. Ni kocha ambaye anatarajiwa kufanya vyema kwenye ligi kuu ya Tanzania hasa kwenye mitaa ya Jangwani.
Kwa upande wa Simba wao wamekuwa na misimu migumu hasa baada ya kuendelea kukosa mataji hasa ya ligi kuu, lakini sasa chini ya kocha mkuu Steve Barker ambaye amejiunga na klabu hiyo akitokea Stellenbosch ya Afrika Kusini na anatarajiwa pia kuleta upinzania mkubwa kabisa kwenye msimu huu.
Hii ni mechi ambayo inakutanisha timu mbili ambazo zinanolewa na makocha ambao wanatoka Afrika Kusini hivyo mbinu ndio zinaweza kuamua nani ataibeba Ngao ya Jamii msimu huu.
Takwimu zinaonesha kuwa mechi 5 za mwisho walizokutana kati ya Simba dhidi ya Yanga Yanga ameshinda mechi 3 na Simba ametoa sare 1 na ameshinda mechi 1, hivyo vijana hawa wa Manqoba ndio wana nafasi nzuri ya kupata matokeo mazuri kutokana na kikosi bora ambacho wanacho.
Timu zote zimefanya usajili mzuri huku upande wa Yanga ameongeza wachezaji kama Peter Shalulile aliyekuwa Mamelodi, Cheikh Ibrahima Touré, Albert Kangwanda kutoka Zambia, Mouhamed Komara kutoka Ivory Coast na wengine wengi ambao wamekuja kuongeza nguvu kikosini hapo.
Lakini bado kwenye klabu hiyo kuna wachezaji tishio na wa kuchungwa Pacome, Nzengeli, Abuya Okelo na wengine huku wakiwa na kipa mzuri Diara. Je Nani kuondoka na ushindi siku ya leo?. Odds Kubwa zipo kwenye mechi hii sasa.
Kwa upande wa Simba wao baadhi ya wachezaji ambao wamewaongeza ni pamoja na Ibrahim Doumbia kutoka Mali, Keletso kutoka Sekhukhune United, Ibraheem Jabaar kutoka Stellenbosch, Nathaniel Chilambo kutoka Azam , Kelvin Nashon ambao nao wamekuja kuungana na wachezaji waliopo kusaka mataji.
Pia nao Simba wana wachezaji wakuchungwa wakiwemo, Mpanzu, Chama, Gueye, Kagoma na wengine wengi. Hivyo kwa ujumla timu ambayo itajiandaa vyema ndio ambayo itaondoka na ushindi. Jisajili hapa na ubeti leo.
