Simba SC yawasili Zanzibar Agosti 10,2026

RASMI kikosi cha Simba SC Agosti 10,2026 kimewasili Zanzibar kwa maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga SC.

Agosti 12,2026 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwa watani hawa wa jadi kuwa uwanjani kupambania taji ya Ngao ya Jamii.

Miongoni mwa wachezaji waliopo katika msafara ni Ibrahim Doumbia, Rushine De Reuck, Ellie Mpanzu, Kibabage, Duchu, Abraham Morice, Libasse Gueye, Clatous Chama, Shomari Kapombe, Neo Maema, Hussen Abel.

Mchezo ujao ni ishara kufungua pazia la NBC Premier League na mabingwa watetezi ni Yanga SC ambao nao wanatarajia kuwasili Zanzibar leo.

Huu utakuwa mchezo wa pili mara baada ya Simba SC kurejea kutoka Rwanda ilipoweka kambi kwa maandalizi ya msimu wa 2026/27.

Mchezo wa kwanza walicheza dhidi ya Police Kenya katika Simba Day, Agosti 8,2026 walipoteza dakika ya 90+1 kwa kufungwa bao moja na Elvins Rupia.

Kwenye Kagame waliishia nafasi ya pili hatua ya makundi, mechi tatu walizocheza ushindi mchezo mmoja dhidi ya Singida Black Stars na waliambulia sare kwenye mechi mbili.

…

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.