SADIO MANE AREJEA SENEGAL

NYOTA wa kikosi cha Liverpool kinachoshiriki Ligi Kuu England, Sadio Mane na mlinda lango namba moja wa Chelsea Eduardo Mendy wamesafiri pamoja kurejea nyumbani Afrika kwa ajili ya kujiunga na timu ya taifa ya Senegal tayari kwa michuano ya AFCON.

Nyota hao walicheza kwenye mchezo wa jumapili wa ligi kuu soka nchini England Chelsea walipowaalika Liverpool.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Stamford Bridge, walitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 na kugawana pointi moja na Mane alikuwa ni miongoni mwa nyota waliotupia kwa Liverpool na bao jingine lilifungwa na Mohamed Salah.

Senegal ni wanafainali waliopita wa michuano ya AFCON walipopoteza kwa kufungwa na Algeria timu zilizokuwa kwenye kundi moja na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwenye michuano hiyo