NENO LA KWANZA LA MRITHI WA MIKOBA YA HAJI MANARA SIMBA

IKIWA ni saa kadhaa kuyeyuka baada ya Ahmed Ally kutanagzwa rasmi kuwa Ofisa Habari wa Simba akichukua mikoba iliyoachwa na Haji Manara ambaye kwa sasa yupo ndani ya Yanga, ameweka wazi malengo ya timu hiyo kuelekea Kombe la Mapinduzi.

Simba ina kazi ya kusaka taji la Mapinduzi ambalo lipo mikononi mwa Yanga ambayo ilitwaa mwaka 2021 kwa ushindi wa mikwaju ya penalti mbele ya Simba.

Ally amesema kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram:”Safari kuelekea Zanzibar. Safari kwenda kuchukua Kombe la Mapinduzi.

“Yes, (ndio) ni rahisi na inawezekana tupo tayari.Tunafahamu wengine hili ndo Kombe lao pekee la kujivunia hivyo tunalichukua Ili tuwakumbushe kuwa sisi ni Wakubwa kwao.

“Saa 8:20 Insha Allah, nitakuwa Forodhani na baadaye saa 11:15 nitahudhuria mazoezi ya kwanza ya timu katika Uwanja wa Mao tse Tung,”.

Simba inatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza Januari 5 dhidi ya Selem View.