ARSENAL V LIVERPOOL YAAHIRISHWA

MCHEZO wa nusu fainali ya Carabao Cup kati ya Arsenal na Liverpool uliopangwa kuchezwa leo Alhamis Januari 6 umeahirishwa kutokana na kuongezeka kwa wimbi la UVIKO-19.

Mchezo huo ulipangwa kuchezwa Uwanja wa Emirates ambapo baada ya kuahirishwa utapangiwa siku nyingine.

Liverpool ilipeleka maombi yao kwa FA kutaka mchezo huo uahirishwe kutokana na wachezaji wake wengi wa kikosi cha kwanza pamoja na benchi la ufundi kubainika kwamba wamepata maambukizi ya Corona.

Wachezaji wenye Uviko-19 ni Robert Firmino, Joel Matip, Allison Becker na Thiago Alcantara. Kocha mkuu Jurgen Klopp na msaidizi wake Pep Lijnders. Mchezo huo umeahirishwa hadi itakapopangiwa tarehe nyingine.