Home International LUKAKU AOMBA RADHI CHELSEA

LUKAKU AOMBA RADHI CHELSEA

STAA wa Klabu ya Chelsea inayoshiriki Ligi Kuu England, Romelu Lukaku amejitokeza hadharani na kuomba radhi kwa mashabiki wa timu hiyo pamoja na kocha wake.

Nyota huyo hivi karibuni alitibua hali ya hewa kwa kuwa aliweka wazi kwamba hafurahishiwa na maisha ndani ya timu hiyo na hakuwa na furaha kabisa.

Lukaku alizua taharuki alipokuwa akifanya mahojiano na aliweka wazi kwamba hana furaha jambo ambalo lilizua mijadala na kuwa gumzo kila kona kutokana na suala hilo hasa kumtaja na kocha kabisa bila hofu.

Jambo ambalo alikuwa haelewi ni mfumo ambao unatumiwa na Kocha Mkuu, Thomas Tuchel ambaye anainoa timu hiyo kwa sasa.

“Naomba msamaha kwa mashabiki wangu kwa yale ambayo yalitokea. Mnafahamu uhusiano wangu na klabu hii tangu nikwa mdogo ila najua mmekasirika juu yangu ni kazi kwangu sasa kurudisha uaminifu kwenu ila nitabadilika na kuhakikisha kuwa naendelea kuwa bora uwanjani,”anesema Lukaku raia wa Ubelgij

Previous articleARSENAL V LIVERPOOL YAAHIRISHWA
Next articleVIDEO:ISHU YA USAJILI YANGA KOCHA AFUNGUKA NAMNA HII