>

MASTAA MANCHESTER UNITED 17 WANATAKA KUSEPA

MANCHESTER United ipo katika wakati mgumu hasa kutokana na kudaiwa kuwa kuna wimbi kubwa la wachezaji wanataka kuondoka wakati huu wa Januari au mwishoni mwa msimu huu.

 

Kwa ufupi ni kuwa kuna hali tete ndani ya Old Trafford, ambapo inaelezwa kuwa kuna wachezaji takribani 17 ambao wanaweza kuondoka.

 

Morali ndani ya klabu hiyo ipo chini licha ya kuwa kuna ujio wa Kocha Ralf Rangnick ambaye ameshindwa kuamsha morali tangu kuondoka kwa Ole Gunnar Solskjaer. Baadhi ya wachezaji wanaoweza kuondoka kwa asilimia kubwa ni wale ambao hawana furaha na mikataba yao inaelekea mwishoni.

 

Baadhi ya wachezaji wanaotajwa kuwa wapo njiani kuondoka ni Anthony Martial, Paul Pogba, Edinson Cavani,
Jesse Lingard, Juan Mata, Donny van de Beek, Dean Henderson, Eric Bailly na Phil Jones. Wengine ni Nemanja Matic, Fred, Diogo Dalot na Axel Tuanzebe.