Home International RUDIGER APELEKWA MAN U

RUDIGER APELEKWA MAN U

BEKI wa zamani wa Manchester United Paul Parker anaamini kama beki wa Chelsea, Antonio Rudiger angetua kikosini hapo basi huenda angekuwa msaada mkubwa.

Nyota huyo kuelekea Januari mwakani atakuwa huru kuzungumza na timu yoyote ambayo itakuwa inahitaji huduma yake.

Mkataba wake ndani ya Chelsea kwa sasa upo ukingoni kumeguka na mabosi wa timu hiyo nao wamekuwa wakitajwa kuanza kufanya naye mazungumzo ili kumuongezea kandarasi mpya.

Beki huyo mkongwe amesema:”Kama atabaki ndani ya Chelsea ni sawa kwani ni mchezaji mzuri ambaye wengi wanamuangalia kutokana na aina ya uchezaji wake.

“Ila kama akija Manchester United litakuwa ni jambo zuri sana pia nitaelewa kwa nini amekuja kwa sababu atataka kuonyesha tofauti kwenye eneo la ulinzi,”.

Previous articleMASTAA YANGA WAIPIGA MKWARA BIASHARA UNITED
Next articleKIKOSI CHA YANGA KITAKACHOANZA DHIDI YA BIASHARA UNITED