Home Sports MASTAA YANGA WAIPIGA MKWARA BIASHARA UNITED

MASTAA YANGA WAIPIGA MKWARA BIASHARA UNITED

MASTAA wa Yanga wameweka wazi kuwa watakachowafanyia Biashara United ni kuchukua pointi zao tatu kwa ajili ya kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa msimu huu.


Yanga kwa sasa ni
vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa wamejikusanyia jumla ya alama 23 mara baada ya kushinda michezo saba na kutoa sare miwili katika michezo tisa ambayo wamecheza mpaka sasa.

Yanga leo Jumapili Desemba 26, wanatarajiwa kumenyana na Biashara United katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Fiston Mayele amesema kuwa ushindi ambao waliupata dhidi ya Tanzania Prisons unawafanya kupata morali ya kuendelea kupata ushindi katika mchezo wao dhidi ya Biashara huku akiweka wazi kuwa malengo yao msimu huu ni kuhakikisha
wanatwaa ubingwa wa ligi 
hiyo.

“Ushindi uliopita ugenini dhidi ya Prisons ulikuwa muhimu kwetu na utatusaidia kupata morali ya kuweza kupata matokeo katika mchezo wetu unaofuata dhidi ya Biashara United.


“Malengo yetu ni yaleyale 
ubingwa msimu huu, kwa sisi wachezaji wageni tunafahamu kabla hata ya kuanza kucheza kuwa malengo msimu huu ni ubingwa, ndio maana kila mchezo kwetu tunauangalia kwa umakini kwa ajili ya kukusanya pointi nyingi zaidi.”

 

Naye kiungo wa timu hiyo, Feisal Salum ‘Fei Toto’, alisema: “Matokeo ya ushindi katika mchezo dhidi ya Biashara United ni ya muhimu kwetu, ili tuweze kutimiza malengo yetu, tunahitaji kushinda sana zaidi ya wapinzani wetu hivyo tutapigania ushindi ili kuweza kufikia malengo yetumsimu huu.”

Previous articleBARBARA AWAPONGEZA WACHEZAJI WAKE
Next articleRUDIGER APELEKWA MAN U