>

KOCHA MANCHESTER UNITED ATAKA VIWANGO KUONGEZEKA

RALF Rangnick, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa ni lazima viwango vya wachezaji wake kuongezeka katika mechi zijazo.

Maneno hayo ameyasema baada ya ubao wa Uwanja wa St James Park kusoma Newcastle United 1-1 Manchester United.

Ni Allan Saint-Maximin alipachika bao la kuongoza kwa timu ya Newcastle dk 7 likasawazishwa dakika ya 71 na Edinson Cavan.

United inafikisha pointi 28 ikiwa nafasi ya 7 huku Newcastle United ikiwa na pointi 11 nafasi ya 19.

Kocha huyo amesema:”Tumepata pointi sawa lakini kwa wachezaji ni muhimu kuweza kuongeza viwango kwenye mechi zijazo ili kupata ushindi,”.