
SUALA LA SIMBA KUMSAJILI MNIGERIA PICHA LIPO HIVI
KIUNGO Mnigeria, Udoh Etop David, amethibitisha kwamba, hajafanikiwa kupata mkataba wa kuitumikia Simba baada ya kufanya majaribio kwa takribani wiki moja. Udoh akiwa kwenye majaribio hayo, alifanikiwa kucheza mechi mbili za Kombe la Mapinduzi, lakini ameshindwa kumshawishi Kocha Pablo Franco. kiungo huyo mkabaji, amesema licha ya kutarajia kupewa mkataba na timu hiyo, lakini hajafanikiwa na kwa sasa kitu ambacho anatarajia ni mipango ya safari yake kutoka Tanzania kurudi kwao Nigeria. “Maisha ya Tanzania ni mazuri na…