Home International ISHU YA MARTIAL KUGOMA KUCHEZA MANCHESTER UNITED AFUNGUKA

ISHU YA MARTIAL KUGOMA KUCHEZA MANCHESTER UNITED AFUNGUKA


ANTHONY Martial, mshambuliaji wa Manchester United amekanusha madai ya Kocha Mkuu Ralf Rangnick kwamba hakutaka kuwa sehemu ya kikosi kilichotoka sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Aston Villa.
Martial anataka kuondoka ndani ya Manchester United na timu unayotajwa kuisaka saini yake ni Sevilla ambayo inahitaji kupata huduma yake.
Katika Uwanja wa Villa Park, United ilikuwa na wachezaji nane benchi kisha baadaye Rangnick aliweka wazi kuwa Martial hakutaka kuwa sehemu ya kikosi.
“Hakutaka kuwa sehemu ya kikosi, kwa kawaida angekuwepo lakini hakutaka hiyo ni sababu ambayo hakusafiri nasi,”.
Martial raia wa Ufaransa kupitia katika mitandao aliandika,”Kamwe sitaweza kukataa kuichezea Man United. Nimekuwa hapa kwa miaka 7 na sijawahi na sitawahi kutoiheshimu klabu na mashabiki,”.
Previous articleYANGA YASEPA NA POINTI TATU MAZIMA MBELE YA COASTAL UNION
Next articleSUALA LA SIMBA KUMSAJILI MNIGERIA PICHA LIPO HIVI