YANGA imesepa na pointi zote tatu mazima mbele ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Ni mabao ya Fiston Mayele dakika ya 40 na lile la pili ni Said Ntibanzokiza ambaye alipachika bao hilo dakika ya 89.
Nyota wa Coastal Union waliweza kwenda mapumziko wakiwa wameokota bao moja nyavuni na waliporudi tena kipindi cha pili wakiokota bao moja.
Ushindi huo unaifanya Yanga kuzidi kujikita nafasi ya kwanza kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 12 na pointi zao ni 32.