>

CHAMA HESABU ZAKE NI MAKOMBE

CLATOUS Chama, nyota wa Simba amesema kuwa ni furaha kwame kurejea ndani ya timu hiyo.

Chama aliibuka ndani ya RS Berkane msimu wa 2021/22 akitokea Klabu ya Simba na amerejea tena nyumbani.

Ni usajili wa kwanza katika dirisha dogo na anatarajiwa kuwa kwenye kikosi cha kesho kitakachomenyana na Mbeya City Uwanja wa Sokoine.

Nyota huyo amesema:”Nafurahi kurejea Simba, nimerudi nyumbani na nina amini kwamba tutapambana kuchukua makombe,”.