Home Sports KOCHA SIMBA AIBUKIA YANGA

KOCHA SIMBA AIBUKIA YANGA

MILTON Nienov aliyekuwa kocha wa makipa ndani ya Simba kabla ya kuchimbishwa leo Januari 16 ametambulishwa ndani ya Yanga.

Nienov anakwenda kuchukua mikoba ya Razack Siwa ambaye anainoa timu hiyo kwa sasa.

Kocha huyo raia wa Brazil aliweka wazi kuwa anaipenda Tanzania kutokana na ukarimu pamoja na mazingira mazuri.

Alikuwa akimnoa Aishi Manula na sasa atakuwa anamnoa Aboutwalib Mshery na Diarra Djigui makipa wa Yanga.

Previous articleBREAKING:YANGA YAMALIZANA NA KIUNGO WA KAZI
Next articleCHAMA HESABU ZAKE NI MAKOMBE