Chico Ushindi ni Mwananchi baada ya kutambulishwa rasmi leo kuwa ndani ya kikosi hicho.
Kiungo huyo mshambuliaji alikuwa anakipiga ndani ya kikosi cha TP Mazembe.
Ametambulishwa rasmi leo Januari 16,2022 ambapo timu ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu Nasreddine Nabi raia wa Tunisia.
Anaungana na wachezaji wengine ambao ni Salim Aboubakhari, Aboutwalib Mshery na Dennis Nkane ambao nao ni maingizo mapya.
Chiko amepewa dili la miaka miwili kuitumikia Yanga.