>

CHAMA HUYO KWENYE MSAFARA WA KUIVAA MBEYA CITY

KIKOSI cha Simba leo Januari 15 kimewafuata Mbeya City kamili kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine.

Januari 17, Simba itakaribishwa na Mbeya City kwenye mchezo huo ambao unasubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki.

Miongoni mwa nyota wa Simba ambao wapo kwenye msafara huo ni pamoja na Clatous Chama ambaye amerejeshwa kwa mara nyingine katika kikosi hicho.

Chama ni usajili wa kwanza ndani ya Simba kwenye dirisha dogo ambalo linatarajiwa kufungwa leo baada ya kufunguliwa Desemba 16,2021.