>

YANGA,SIMBA MNASTAHILI PONGEZI KWA KUREJESHA KWA JAMII

PONGEZI kwa watani wa jadi Yanga na Simba kwa kuwa na desturi ya kutembelea wahitaji na kuwajulia hali ni jambo la kiungwana.

Jambo hili linapaswa kuwa na mwendelezo kila wakati ili kuwa karibu zaidi na jamii ambao ni wadau na mashabiki wa timu zote Bongo.

Yanga wamekuwa na desturi ya kuwatembelea wahitaji na kuwa karibu nao kwenye kila safari ambazo wanazifanya Dar na mikoani pia hasa wakiwa na mechi katika sehemu husika.

Walifanya hivyo pia hata walipokuwa Zanzibar katika Kombe la Mapinduzi pongezi katika hilo

Pia leo Januari 15 taarifa ambayo imetolewa na Yanga imeeleza kuwa walipata nafasi ya kuitembelea Taasisi ya Elimu na Maarifa ya Dini ya Kiislaam Mahaad Shamsil Maarif Islamiyah iliyopo Tanga.

Pia Simba nao leo Januari 15,2,2022 kabla ya kuondoka kuelekea Mbeya wachezaji walitembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika ICU ya watoto kumjulia hali Bakari Juma Seleman,(13).

Bakaru anaugua maradhi ya Autoimmune Disease inayopelekea misuli ya mwili kupooza na amelazwa hapo kwa zaidi ya miezi miwili na aliomba kuonana na wachezaji wa Simba.

Kila la kheri kwa wale ambao afya zao hazijatengamaa.