>

SIMBA WAMFANYIA HAYA KIUNGO CHAMA

UKISIKIA watu wanakwambia Simba wamefanya kufuru, basi amini kwamba ufanikishaji wa kuipata saini ya kiungo
Mzambia, Clatous Chama 
imetumika gharama kubwa sana.


Chama ambaye 
amerejea Simba na kusaini mkataba wa miaka miwili, aliondoka kikosini hapo Agosti 2021, baada ya kuisaidia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara tatu mfululizo kuanzia msimu wa 2018/19 hadi 2020/21
na kutua RS Berkane ya 
Morocco.


Pia Chama alikuwepo 
kwenye kikosi cha Simba kilichocheza hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara mbili msimu wa 2018/19 na 2020/21.


Kiungo huyo baada 
ya kutua RS Berkane, amefanikiwa kukaa huko kwa takribani miezi mitano kabla ya kurudi Simba.


Chanzo chetu cha 
kuaminika kutoka ndani ya Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, kimeliambia Spoti Xtra kwamba,
dau la usajili wa Chama 
limegharimu dola 150,000 (sawa na Sh 344,697,000 za Kitanzania).


Mtoa taarifa huyo 
aliongeza kwamba, mshahara wake kwa mwezi ni dola 15,000 (sawa na Sh 34,469,700
za Kitanzania) ambapo 
ndani ya miaka miwili ikiwa na jumla ya miezi 24, atalipwa Sh 827,272,800 za Kitanzania.