
WASHIKA BUNDUKI WAKIWASHA HUKO LIGI KUU ENGLAND
BUNDUKI za washika bunduki Klabu ya Arsenal ziliweza kujibu kwa furaha baada ya kuwatungua Aston Villa katika mchezo wa Ligi Kuu England mabao 3-1 na kuwafanya waweze kusepa na pointi tatu mazima. Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Emirates vijana wa Kocha Mkuu, Mikel Arteta walitawala kila idara huku mabao yao yakipachikwa na Thomas Partey…