RAMADHAN Nswazurimo, Kocha Mkuu wa Klabu ya DTB inayoshiriki Championship ameweka wazi kuwa mshambuliaji wake Amisi Tambwe anaweza kutwaa tuzo ya ufungaji bora.
Tambwe kwa sasa anakimbiza kwa kucheka na nyavu akiwa na mabao sita, aliweza kuzifunga African Lyon mabao manne,Green Warrior bao moja na bao lake la sita aliwatungua African Sports.
Akizungumza na Saleh Jembe, Nswanzirimo amesema kuwa kwa namna kasi ya Tambwe inavyokwenda na ushirikiano kutoka kwa wachezaji wengine anaweza kuwa mfungaji bora.
“Naona kabisa anaweza kuwa mfungaji bora lakini nataka kuona anafanya jitihada zaidi kila anapopata nafasi na kushirikiana na wengine, uhakika zaidi wa kuwa na hiyo tuzo ni pale ambapo atafanya kazi kwa juhudi.
“Ligi ni ngumu nasi tunapambana ili kupata matokeo hivyo mashabiki wazidi kuwa nasi bega kwa bega kwa kuwa malengo yetu ni kupata matokeo,” .
Mchezo ujao kwa DTB ni dhidi ya JKT Tanzania ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Isamuhyo itakuwa Oktoba 23.