>

REKODI ZA AIR MANULA BONGO ZIPO NAMNA HII

AISHI Manula, anapenda kujiita Air Manula kipa namba moja wa Simba amezidi kuwa bora langoni ambapo mpaka sasa kwa rekodi zake hakuna kipa ndani ya Ligi Kuu Bara ambaye ameweza kumfikia na ni yeye amesepa na tuzo yake ya kipa bora kwa msimu wa 2020/21.

Aliweza kuwashinda Jeremiah Kisubi ambaye alikuwa Tanzania Prisons na sasa yupo ndani ya Klabu ya Simba pamoja na Haroun Mandanda wa Mbeya City.

Msimu wa 2020/21 katika mashindano yote ikiwa ni kuanzia kwenye ligi, Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa Afrika alikaa langoni kwenye mechi 45 alifungwa jumla ya mechi 17 mabao 21 na kukusanya clean sheet 28.

Kwenye ligi alidaka mechi 29 kati ya 34 na alifungwa kwenye mechi 11 mabao 12 na alikusanya jumla ya clean sheet 18.

Alizotunguliwa hizi hapa:-Ihefu 1-2 Simba, Mtibwa Sugar 1-1 Simba, Prisons 1-0 Simba, Yanga 1-1 Simba, Dodoma Jiji 1-2 Simba,Simba 2-2 Azam FC,Simba 1-1 Prisons, Simba 3-1 Dodoma Jiji,Namungo 1-3 Simba, Simba 4-1 Mbeya City na Simba 0-1 Yanga.

Clean sheet 18 zake :-Simba 4-0 Biashara United, Simba 3-0 Gwambina, JKT Tanzania 0-4 Simba, Coastal Union 0-7 Simba, Simba 2-0 Polisi Tanzania, Mbeya City 0-1 Simba, Simba 1-0 KMC.

Simba 4-0 Ihefu, Biashara United 0-1 Simba, Simba 3-0 JKT Tanzania, Simba 5-0 Mtibwa Sugar, Mwadui 0-1 Simba, Kagera Sugar 0-2 Simba, Gwambina 0-1 Simba, Ruvu Shooting 0-3 Simba, Polisi Tanzania 0-1 Simba, KMC 0-2 Simba, Simba 4-0 Namungo.

Kimataifa

Kimataifa alikaa langoni kwenye mechi 11 alikusanya clean sheet 7 alifungwa mabao 7 kwenye mechi nne. Alipata tabu ilikuwa FC Platinum 1-0 Simba, Simba 4-1 AS Vita, Al Ahly 1-0 Simba, Kaizer Chiefs 4-0 Simba.

Clean sheet zake hizi hapa:-Plateau United 0-1 Simba,Simba 0-0 Plateau United,Simba 4-0 FC Platinum,AS Vita 0-1 Simba, Simba 1-0 Al Ahly, Simba 3-0 Al Merrikh na Simba 3-0 Kaizer Chiefs.

Kombe la Shirikisho

Katika Kombe la Shirikisho, (FA) alicheza mechi tano na alikusanya clean sheet tatu ilikuwa mbele ya African Lyon 0-3 Simba, Azam FC 0-1 Simba na Yanga 0-1 Simba. Alifungwa kwenye mechi mbili mabao mawili ilikuwa Simba 2-1 Kagera Sugar na Simba 3-1 Dodoma Jiji.

Msimu huu wa 2021/22 tayari amekaa langoni kwenye mechi 6 na kutumia dakika 540,alicheza bila kufungwa , (Clean Sheet) 4 mechi zake ilikuwa, Biashara United 0-0 Simba, Dodoma Jiji 0-1 Simba, Benin 0-1 Tanzania, Jwaneng 0-2 Simba.Kuruhusu mabao mechi mbili ilikuwa namna hii Simba 0-1 Yanga na Taifa Stars 0-1 Benin.

Didier Gomes, Kocha Mkuu wa Simba alisema kuwa Manula amekuwa akiimarika kila leo na hata anapokuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa huwa anafanya kazi nzuri.