>

KWA KUITUNGUA UNITED,DAKA APEWA TANO NA RAIS

HAKAINDE Hichilema, rais wa Zambia amempongeza kijana wake anayekipiga ndani ya Leicester City, Patson Daka kwa kuwatungua Manchester United kwenye ushindi wa mabao 4-2 katika mchezo wa Ligi Kuu England.

 

Hichilema ameweka wazi kuwa kazi ambayo imefanywa na Mzambia huyo ni nzuri na wanajivunia kuwa na kijana ambaye anatimiza majukumu yake kwa umakini jambo ambalo lilimpa tabasamu Daka aliyeweka wazi kuwa anafurahia sapoti kubwa kutoka kwa mheshimiwa rais.

Hichilema amesema:”Kijana unastahili pongezi kwa kuwa unafanya kazi kwa umakini kuiwakilisha Namibia katika anga za kimataifa,”.

Kwenye mchezo huo watikisa nyavu kwa upande wa Leicecter City walikuwa ni Youri Tielemans dakika ya 31,Caglar Soyuncu dakika ya 78, Jamie Vady dakika ya 83 huku Mzambia huyo akipachika msumari wake wa mwisho dakika ya 90 na alikuwa ametoka kusugua benchi.

Mason Greenwood dakika ya 19,Marcus Rasford dakika ya 82 hawa walifunga kwa upande wa Manchester United kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa The King Power, Oktoba 16.

Mzambia huyo amesema:”Nashukuru kupewa hongera kwa hilo kwa kuwa ni jambo kubwa na zuri,”.