Home Sports SIMBA YAWAVUTIA KASI WABOTSWANA

SIMBA YAWAVUTIA KASI WABOTSWANA

KIKOSI cha Simba leo Oktoba 22 kimeendelea kuivutia kasi timu ya Jwaneng Galaxy ya Botswana kuelekea kwenye mchezo wao wa marudio wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Oktoba 24.

Miongoni mwa nyota ambao walikuwepo kwenye mazoezi ya leo yaliyofanyika Uwanja wa Boko Veterani, Bunju ni pamoja na kiungo mkata umeme mpaka nguzo wa kumuita Taddeo Lwanga, Yusuf Mhilu, mshambuliaji Meddie Kagere na nahodha John Bocco.

Simba itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa awali uliochezwa nchini Botswana hivyo wana kazi kubwa ya kulinda ushindi huo wakiwa nyumbani.

Akizungumza na Saleh Jembe, nahodha msaidizi wa Simba, Shomari Kapombe ambaye jina lake lipo kwenye orodha ya kikosi bora cha Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo.

“Tunajua kwamba utakuwa mchezo mgumu lakini tupo tayari, sisi wachezaji na kila mmoja anatambua kwamba ni lazima tucheze kwa umakini na kwa hesabu ili kupata ushindi.

“Mashabiki wajitokeze kuona namna ambavyo tutafanya kwani wamekuwa ni furaha kwetu kwa namna ambavyo wamekuwa pamoja nasi kila wakati,” amesema Kapombe.

Previous articleTAMBWE APEWA TUZO YA UFUNGAJI BORA
Next articleTWIGA STARS YAKIRI KUFANYA MAKOSA,KESHO KUFANYA KWELI