KOCHA wa Timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars, Bakari Shime, amesema walifanya makosa
kwenye mchezo uliopita wakiwa nyumbani na sasa wanakwenda kuwafunga Namibia wakiwa kwao, kesho Jumamosi.
Twiga Stars walichapwa 2-1 na Namibia kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kwenda Afcon
mwakani, kwenye mtanange uliochezwa Jumatano Uwanja wa Mkapa, Dar.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Shime alisema walifanya makosa kwenye mchezo uliopita, wameliona hilo na watakwenda kulifanyia kazi wakiwa ugenini ambako kwa namna yoyote lazima wapate ushindi.
Tayari kikosi cha Twiga Stars kipo nchini Namibia na kimefanya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mchezo huo unaoatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.