Home Sports SIMBA YASAHAU MATOKEO YA BOTSWANA,KAZI KESHO

SIMBA YASAHAU MATOKEO YA BOTSWANA,KAZI KESHO

SHOMARI Kapombe, beki wa Klabu ya Simba ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana huku wakiwa wamesahau matokeo ya mchezo wao uliochezwa nchini Botswana.

Oktoba 17 kikosi hicho kiliweza kushinda mchezo wa mtoano jambo ambalo linawapa nguvu ya kujiamini kuelekea kwenye mchezo wao ujao ambao ni wa marudio wakiwa nyumbani, Uwanja wa Mkapa.

Kesho, Oktoba 24 Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa mtoano na ikiwa itashinda itatinga hatua ya makundi.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Botswana ubao ulisoma Jwaneng Galaxy 0-2 Simba na mabao yalifungwa na John Bocco na Taddeo Lwanga.

Kapombe amesema:”Tupo tayari kwa ajili ya mchezo na kikubwa ni kuona tunapata ushindi,tunajua kwamba itakuwa kazi kubwa na ngumu lakini matokeo ya ugenini tumeyasahau hatupo na matokeo ya Botswana.

“Jambo moja ambalo tunahitaji ni ushindi tunajua kwamba hata mashabiki wanahitaji hilo tutapambana ili kufanya vizuri na kila kitu tunaamini kitakuwa sawa,”.

Previous articleKUMBE FATI ALITAKA KUONDOKA BARCELONA
Next articleWASHIKA BUNDUKI WAKIWASHA HUKO LIGI KUU ENGLAND