STAA wa Barcelona, Ansu Fati ameweka wazi kuwa ilibaki kidogo kusepa ndani ya timu hiyo kwa kuwa alipata ofa nyingi sana lakini akaamua kubaki ndani ya timu hiyo inayoshiriki La Liga.
Nyota huyo amekubali kusaini dili jipya kuitumikia timu hiyo na sasa dau lake la usajili lilikuwa ni Euro bilioni moja mkwanja ambao sio wa kitoto.
Kinda huyo anatajwa kuwa anapaswa kuwa maarufu kama ilivyokuwa nyota wao wa zamani Lionel Messi ambaye kwa sasa anakipiga ndani ya PSG ya Ufaransa.
Fati amesema:”Kulikuwa na ofa nyingi sana kabla sijakubali kusaini Barcelona tena kwa kipindi cha miaka sita lakini awali nilishamwambia wakala wangu kwamba nataka kubaki hapa,”.