BONGO ZOZO AMPA TUZO YAKE HAJI MANARA

BONGO Zozo amesema kuwa ingekuwa ni suala la yeye kuchagua nani angempa tuzo ambayo ameipokea katika kipengele cha Mhamasishaji Bora angempa Haji Manara.

Kwenye tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) zilizopewa jina la usiku wa Tuzo za TFF 2021 Tuzo ya Mhamasishaji Bora ilikwenda kwa Nick Leonard, ‘Bongo Zozo’.

Bongo Zozo amebainisha kuwa hakutarajia kutwaa tuzo hiyo kwa kuwa alikuwa anashindanishwa na watu imara na wanaofanya kazi kwa umakini.

Alikuwa anapambanishwa na Haji Manara ambaye alikuwa Ofisa Habari wa Simba ila kwa sasa maisha yake yapo ndani ya kikosi cha Yanga akiendelea maisha yake kama kawaida na mwingine ni Masau Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting.

Masau Bwire bado yupo ndani ya Ruvu Shooting akiendelea kutimiza majukumu yake alikuwepo kwenye Usiku wa Tuzo ambapo alimshuhudia Bongo Zozo akisepa na tuzo hiyo.

Bongo Zozo amesema:”Ingekuwa ni mimi ninatoa tuzo ningempatia Haji Manara kwa sababu ni mtu ambaye ninamkubali na anafanya kazi yake vizuri.

“Lakini kwa kuwa mimi nimepewa basi hakuna namna walionipa wanajua kile ambacho nimekifanya na katika hilo ninashukuru kwa kuwa tuzo ni kitu kikubwa,”.