>

FEI TOTO ATOA SIRI YA MABAO YA KIDEONI

KIUNGO mzawa wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’, amebainisha kuwa amezoea kufunga mabao magumu jambo ambalo halikumpa shida kuwatungua KMC.

 

Nyota huyo ambaye juzi Jumanne alifunga bao la kideoni nje ya 18 na kutoa asisti katika ushindi walioupata Yanga wa mabao 2-0, amesema ataendelea kufunga kwa staili hiyo kila akipata nafasi.

 

Akizungumza na Spoti Xtra muda mfupi baada ya kutua Dar wakitokea Songea, Fei Toto alisema: “Mchezo ulikuwa mgumu na uwanja haukuwa rafiki kwetu katika kusaka ushindi.

“Kuhusu bao ambalo nilifunga ni kawaida yangu kufunga vile na nimezoea kwa sababu huwa ninafanya mazoezi sana.

 

“Bao lile ni zawadi kwa mama kwa sababu ninampenda, amekuwa na mchango mkubwa kwenye mafanikio yangu na kazi yangu pia.

 

“Ilikuwa ngumu kumfunga Shikhalo (Faroukh) kwa kuwa anatujua vizuri, lakini wachezaji tulikuwa na jukumu la kutafuta ushindi.”

 

MANARA: BAO LA FEI TOTO LIPEWE TUZO YA DUNIAKwa upande wa Msemaji wa Yanga, Haji Manara, alisema kuwa bao la Fei Toto ni moja ya bao bora na ikiwezekana lipewe Tuzo ya Dunia.

 

“Ni bao bora sana, linafaa kuwania Tuzo ya Bao Bora lililofungwa mwezi huu kwenye mechi zote duniani, hakuna mchezaji aliyefunga kama lile.“Unajua kupiga shuti kama lile uwe na uhakika wa kula kama mara nne au tano kwa

siku.”Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mazingiza, alisema baada ya mchezo huo, akili zao wanazielekeza mechi zijazo ikiwa dhidi ya Azam FC itakayochezwa Oktoba 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

“Tumemaliza kazi mbele ya KMC, sasa akili yetu ni kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Azam FC, tunajua kwamba utakuwa mchezo mgumu lakini tupo tayari.”