
KIKOSI CHA YANGA KITAKACHOANZA DHIDI YA BIASHARA UNITED
KIKOSI cha Yanga leo Desemba 26 kitakachoanza dhidi ya Biashara United, Uwanja wa Mkapa.
KIKOSI cha Yanga leo Desemba 26 kitakachoanza dhidi ya Biashara United, Uwanja wa Mkapa.
BEKI wa zamani wa Manchester United Paul Parker anaamini kama beki wa Chelsea, Antonio Rudiger angetua kikosini hapo basi huenda angekuwa msaada mkubwa. Nyota huyo kuelekea Januari mwakani atakuwa huru kuzungumza na timu yoyote ambayo itakuwa inahitaji huduma yake. Mkataba wake ndani ya Chelsea kwa sasa upo ukingoni kumeguka na mabosi wa timu hiyo nao…
MASTAA wa Yanga wameweka wazi kuwa watakachowafanyia Biashara United ni kuchukua pointi zao tatu kwa ajili ya kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa msimu huu. Yanga kwa sasa ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa wamejikusanyia jumla ya alama 23 mara baada ya kushinda michezo saba na kutoa sare miwili katika michezo tisa ambayo wamecheza mpaka sasa. Yanga leo Jumapili Desemba 26, wanatarajiwa kumenyana na Biashara United katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar….
MTENDAJI Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez ameweka wazi kuwa Simba ipo imara na hesabu kubwa ni kutimiza malengo waliyojiwekea kutokana na wachezaji walionao kujituma. Kwa sasa Simba inapambana kuweza kutetea taji lake ililotwaa msimu uliopita wakivutana kwa kasi na vinara wa ligi ambao ni Yanga wenye pointi 23 huku Simba wakiwa nafasi ya pili na pointi 21. Barbara amesema kuwa wanazidi kufanya mambomazuri kwa ajili ya timu na kwa sasa…
IMEFICHUKA kuwa uongozi wa Klabu ya Yanga umeingilia dili la kumnasa nahodha wa Biashara United, Abulmajid Mangalo ambaye amekuwa akiwindwa kwa ukaribu na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba. Hivi karibuni, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, aliwasilisha ripoti ya usajili ambapo miongoni mwa maeneo ambayo amehitaji yafanyiwe maboreshio ni nafasi ya mlinzi wa kati akitaka beki kuja kuwapa changamoto, Dickson Job na Bakari Mwamnyeto. Mpaka sasa Mangalo amebakisha…
IMEBAINIKA kuwa mabosi wa Simba wapo katika harakati za kumrudisha kiungo mkabaji Gerson Fraga raia waBrazil kwa ajili ya kuziba pengo la kiungo Taddeo Lwanga ambaye amekuwa na majeraha ya mara kwa mara Lwanga ameshindwa kuitumikia Simba katika ligi kuu mara baada ya kuumia katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi Jwaneng Galaxy ambapo katika mchezo huo Simba ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-1. Simba kwa sasa wamekuwa wakiwatumia…
PASCAL Wawa, beki wa kati wa Simba, ameweka wazi kuwa hakuna tofauti kati yake na Kocha Mkuu wa timu hiyo Pablo Franco. Juzi, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ilitokea hali ya kutoelewana katika suala la kufanya mabadiliko ambapo Wawa alikuwa anajiandaa kuingia uwanjani akitokea benchi ghafla, Pablo alimvuta kwa nguvu kubwa na kuonekana akilalamika. Pia…
MSHAMBULIAJI Deo Kanda raia wa Congo amemalizana na timu kongwe ndani ya ardhi ya Tanzania, Mtibwa Sugar kwa ajili ya kutoa huduma kwenye kikosi hicho kwa msimu wa 2021/22. Ikumbukwe kwamba kabla ya Kanda kujiunga na Mtibwa Sugar amezitumikia TP Mazembe, Simba,Raja Casablanca,Vita Club AE Larisa na DC Motema Pembe. Pia alipokuwa ndani ya Simba…
VINARA wa Ligi Kuu Bara, Yanga wameweka wazi kwamba wanahitaji pointi tatu za Biashara United kwenye mchezo wao wa ligi unaotarajiwa kuchezwa leo Uwanja wa Mkapa. Yanga ipo nafasi ya kwanza na pointi zake 23 inatarajiwa kukutana na Biashara United iliyo nafasi ya 14 na pointi 8. Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa…
HEKAHEKA za usajili wa dirisha dogo ndani ya Ligi Kuu Bara zimeanza huku timu nyingi zikianza mikakati ya kuviboresha vikosi vyao kuelekea mzunguko wa pili ili ziweze kufanya vizuri kwenye ligi na michuano mingine ambayo watashiriki. Kipindi hiki timu zinapaswa kuwa makini katika kuhakikisha wachezaji ambao watasajiliwa waendane na mahitaji ya benchi la ufundi…
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Jumapili
Kwa wapenzi wa soka, burudani ndio kwanza inaanza, sikukuu inanoga zaidi ukiwa unautizama mkeka wako unavyokuletea faida ndani ya dakika 90. Hii ndio nyumba ya mabingwa, Meridianbet! Jumapili hii, Manchester City watawaalika Leicester City katika ungwe ya pili ya msimu wa EPL, 2021/22. Safari ya ubingwa inaanza kushika kasi, ni Pep Guardiola vs Brendan…
PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kilichotokea kwenye mchezo wa ligi dhidi ya KMC ni kutoelewana na mwamuzi. Jana Pablo akiwa benchi alionekana kumzuia Pascal Wawa asiweze kuingia kuendelea kutimiza majukumu yake. Kwenye mchezo huo ubao wa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ulisoma KMC 1-4 Simba na kuiwafanya mabingwa hao watetezi kusepa na…
MLINDA mlango namba moja wa Klabu ya Polisi Tanzania, Metacha Mnata rasmi amevunja mkataba na aliyekuwa meneja wake Jemedari Said. Hili limekuja wakati huu ambapo Metacha anazungumzwa kuhitajika na Yanga ambao watakosa huduma ya kipa wao namba moja raia wa Mali Diarra ambaye anakwenda kujiunga na Timu yake ya Taifa katika michuano ya AFCON. Kwa…
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba jana Desemba 24 wametoa zawadi ya Krismasi kwa mashabiki wake baada ya kusepa na pointi tatu mazima mbele ya KMC. Baada ya dakika 90 kukamilika ubao wa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ulisoma KMC 1-4 Simba ikiwa ni ushindi wao wa kwanza kushinda mabao zaidi ya matatu kwenye…
ZAWADI ya Krismasi kwa mashabiki wa Yanga ni saini ya kiungo wa mpira Salum Aboubhakari ambaye alikuwa anakipiga ndani ya Azam FC. Jana, Desemba 24 Sure Boy alitambulishwa Yanga kwa dili la miaka miwili ambao dau lake linatajwa kuwa milioni 80. Ikumbukwe kwamba Sure Boy alisimamishwa kwenye timu yake ya zamani ambayo ameitumikia kwa muda…
REKODI za winga mpya wa Yanga, Chico Ushindi zinatisha jambo ambalo linaonesha ni kweli timuhiyo imepata jembe la maana ambalo litakuja kuongeza makali katika safu ya ushambuliaji ambayo kwa sasa inazidi kuwa kiwembe. Yanga tayari imekamilisha usajili wa mkopo wa winga huyo ambaye alikuwa anakipiga katika Klabu yaTP Mazembe ya nchini DR Congo. Katika mkataba huo, kuna kipengele cha nyota huyo anayetumia miguu yote kusakata kabumbu kujiungana Yanga moja kwa moja kama…