>

JEMBE LA SIMBA LAMALIZANA NA TIMU KONGWE

MSHAMBULIAJI Deo Kanda raia wa Congo amemalizana na timu kongwe ndani ya ardhi ya Tanzania, Mtibwa Sugar kwa ajili ya kutoa huduma kwenye kikosi hicho kwa msimu wa 2021/22.

Ikumbukwe kwamba kabla ya Kanda kujiunga na Mtibwa Sugar amezitumikia TP Mazembe, Simba,Raja Casablanca,Vita Club AE Larisa na DC Motema Pembe.

Pia alipokuwa ndani ya Simba kwenye mchezo wake wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa alikuwa ni mmoja wa nyota waliyezama nyavuni.

Kwenye mchezo huo ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 2-2 Yanga na ilikuwa ni moja ya mechi ya kibabe hivyo kwa sasa ubabe wake utakuwa ndani ya Mtibwa Sugar.

Anaungana na mshikaji wake ambaye walikuwa naye ndani ya Simba, Said Ndemla ambaye ni kiungo yeye ametupia bao moja kwa msimu huu wa 2021/22.

Ni zawadi ya Krismasi kwa mashabiki wa Mtibwa Sugar kwa kuwa alitambulishwa rasmi Desemba 25.