YANGA YAZITAKA POINTI TATU ZA BIASHARA UNITED

VINARA wa Ligi Kuu Bara, Yanga wameweka wazi kwamba wanahitaji pointi tatu za Biashara United kwenye mchezo wao wa ligi unaotarajiwa kuchezwa leo Uwanja wa Mkapa.

Yanga ipo nafasi ya kwanza na pointi zake 23 inatarajiwa kukutana na Biashara United iliyo nafasi ya 14 na pointi 8.

Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga  amesema kuwa kwenye mechi zote ambazo wanacheza wanahitaji kushinda ili kupata pointi tatu.

“Tunajua kwamba tuna mechi nyingi za kucheza na mchezo wetu wa Prisons ulipokamilika unafuata ule dhidi ya Biashara United hakuna namna tunahitaji ushindi.

“Kila mchezaji anajua kwamba ambacho tunatakiwa kukifanya ni kuongeza jitihada na kupata ushindi hakuna jambo lingine,” alisema Nabi.

Kwenye mchezo huo mabao ya Yanga yalifungwa na Feisal Salum kwa pasi ya Khalid Aucho na bao la pili lilifungwa na Aucho kwa pasi ya Said Ntibanzokiza.